22 Septemba 2022 - 16:39
World Islamic Peace Forum: Nchi zote zinapasa kujiunga na Muungano wa Amani Duniani

Jukwaa la Kimataifa la Kiislamu la Amani limetangaza kuwa nchi zote zinapaswa kujiunga na muungano wa amani wa kimataifa kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja duniani.

Katika kalenda ya kimataifa tarehe 21 mwezi Septemba imepewa jina la Siku ya Kimataifa ya Amani. Jukwaa la Kimataifa la Kiislamu la Amani limetoa taarifa kwa mnasaba wa madhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani  na kuitaka siku hii kama fursa kwa ajili ya kuratibu na kubainisha fikra za Kiislamu katika uwanja huo; na kukumbusha mazungumzo ya kiadilifu ya amani kwa mtazamo wa kulinda heshima na utu wa mwanadamu kupitia mazungumzo ya pamoja duniani. 

Taarifa ya World Islamic Peace Forum imebainisha kuwa: kuwa na ulimwengu iliyojengeka katika misingi ya amani, urafiki na uadilifu ni matarajio ya dini,  watu, mataifa na tamaduni zote duniani ambapo kushughulika na masuala ya amani na kupata njia za kufikia suala hilo ni moja ya changamoto kuu zinazomkabili mwanadamu khususan katika ulimwengu wa sasa. Hii ni kwa sababu kivuli cha vita na ugaidi mara nyingi huisika katika maisha ya mwanadamu. 

Taarifa ya Jukwaa la Kimataifa la Kiislamu la Amani imeongeza kuwa: Kwa mujibu wa hati ya Umoja wa Mataifa, umoja huo umetangaza kuwa,lengo lake kuu ni kulinda na kurejesha amani na utulivu duniani; na tokea mwaka 1982 Umoja wa Mataifa umeipa jina siku ya tarehe 21 mwezi Septemba kuwa ni Siku ya KImataifa ya Amani. Aidha siku hii huadhimishwa na mataifa na shakhsia mbalimbali kote duniani kwa shabaha ya kuleta amani na kukomesha machafuko na vita katika pembe mbalimbali duniani. 

Aidha Umoja wa Mataifa mwaka huu umeitaja Siku hii ya Kimataifa ya Amani Duniani kuwa ni kwa ajili ya kuhitimisha ubaguzi wa rangi na kuwa na dunia yenye amani; ambapo Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres amesisitiza kuwa: ubaguzi wa rangi unaendelea kuzitia sumu taasisi na mifumo ya kijamii   katika masiah ya kila siku ya watu.  

342/